![](https://mandelaveteransportsclub.co.tz/wp-content/uploads/2020/11/Capture_1200x740.png)
Kila mwanachama wa Klabu atakuwa na wajibu ufuatao:
- Kulipa kiasi chote cha fedha anachodaiwa na Klabu pamoja na michango
- Kuwa mwaminifu na mtiifu kwa Klabu
- Kukubali kufuata Katiba hii, kanuni, maagizo na maamuzi ya Klabu na ya vyama vya mpira wa miguu (SUFA, FARU na TFF)
- Kufuata kifungu cha sheria kinachoeleza bayana kuwa hatua zote za kisheria zinazohitaji kuamua migogoro inayohusu yeye au mwanachama mwingine na kuhusiana na Katiba, kanuni, maagizo na maanuzi ya Klabu na kwamba ni lazima iwe kwa mujibu wa mamlaka pekee ya Baraza la usuluhishi litakalotoa uamuzi
- Kufuata masharti yaliyobainishwa katika ibara ya 6 katika kipindi chote cha uanachama wake
- Kufuata misingi ya uaminifu, uadilifu na mwendo mzuri wa kimichezo kama kuonyesha mchezo safi
- Wajibu mwingine wowote unaotokana na Katiba hii, kanuni, maagizo na maamuzi ya Mandela Veteran Football Club
Aidha wanachama wataheshimu wajibu ufuatao:
- Watakubaliana kuitumia Bodi ya Utendaji ya Klabu, Kamati ya nidhamu ya Klabu, Kamati ya nidhamu ya TFF na Baraza la usuluhishi la TFF
- Kutopeleka masuala ya mpira wa miguu katika mahakama ya kawaida ya sheria
- Mwanachama au mtu yeyote (mchezaji au kiongozi) atakayetafuta msaada katika mahakama za kawaida ya sheria kuhusu mgogoro unaohusiana na Katiba, kanuni, taratibu, maagizo na maamuzi ya Mandela Veteran Football Club atasababiishwa kusimamishwa mara moja na Bodi ya utendaji
Ibara ya 12: Kupoteza hadhi ya mwanachama
- Hadhi ya mwanachama itakoma kwa kujiuzuru uanachama au kufukuzwa kutokana na ukiukwaji wa kanuni na sheria za katiba hii,TFF na sheria za nchi kwa ujumla.
- Kupoteza uanachama hakutamwondolea mwanachama huyo madeni yake katika Klabu au kwa wanachama wemgine wa chombo hicho
- Kufariki, Mwanachama wa kudumu anapofariki, uanachama wake utakoma, lakini haki zake kikatiba atapewa mrithi wake halali ambaye atakuwa na hiyari ya kuendeleza uanachama kwa kwa mujibu wa masharti haya.
- Kichaa kilichothibitishwa na daktari kama ilivyoelezwa kwenye kipengere cha Ibara ya 6(b).
- Kujiuzulu baada ya kutoa taarifa ya maandishi miezi mitatu kabla, mwanachama wa kudumu anaweza kujitoa mwenyewe kwenye chama kwa sababu atakazoona zinafaa.
- Kwa kujitoa mwenyewe atakuwa amejifuta kwenye uanachama wa kudumu au mkataba na kurudishiwa stahiki zake zote na kila kila kitu alichokuwa anapata kitakoma siku hiyo hiyo.
- Kukataliwa uanachama na theluthi mbili (⅔) ya wanachama waliohudhuria katika Mkutano Mkuu baada ya kupewa nafasi ya kujitetea baada ya kufanya makosa ambayo yanamlazimu kukataliwa uanachama. Mfano Kupigana au tabia zingine zisizokuwa za utu.
- Kufanya kitendo chochote ambacho wanachana na uongozi kwa ujumla wataridhika kuwa ni cha kutokuwa mwaminifu au ambacho ni kinyume na madhumuni ya jumuiya na ambacho kinavuruga malengo ya chama.
- Kutoshiriki katika shughuli za chama kwa muda wa miezi mitatu (3) bila taarifa ya yeyote.
- Mwanachama ambaye uanachama wake umekoma hatarudishiwa kiingilio alichotoa. Iwapo hadaiwi na chama atarudishiwa hisa zake zote baada ya miezi mitatu kupita tangu siku uanachama ulipokoma.
- Kukosa sifa baada ya kushindwa kutimiza masharti ya kulipa michango ya kila mwezi kwa muda wa miezi mitatu (3) mfurulizo.