![](https://mandelaveteransportsclub.co.tz/wp-content/uploads/2020/11/Capturen_1200x740.png)
Kamati ya ufundi na tiba itachambua vipengere vya msingi vya maendeleo ya ufundi ya mchezo wa mpira wa miguu. Itaandaa mpango wa maendeleo, kufuatilia utekelezaji na kufanya tathimini ya mara kwa mara ya mafanikio au vikwazo katika mchezo wa mpira wa miguu na Klabu kwa ujumla. Pia itashughulika na masuala ya jumla yanayohusu maendeleo ya mpira wa miguu na Klabu kwa ujumla
Kamati ya Fedha na Mipango itafuatilia usimamizi wa fedha na kuishauri Bodi ya utendaji kuhusu masuala ya fedha na usimamizi wa rasiliamali fedha na watu. Itachambua bajeti ya Klabu na taarifa za fedha zilizotayarishwa na kuwasilishwa kwa Bodi ya utendaji kwa kuthibitishwa. Pia itapitia mipango ya muda mfupi, wa kati na mrefu wa Klabu. Aidha itashughulikia mikakati ya kitaifa na kimataifa kuhusu mpira wa miguu na hadhi yake, kiuchumi na kijamii