Aina za wanachama
Kutakuwa na aina zifuatazo za wanachama:
- Wanachama waanzilishi. Uanachama utakuwa wa wazi kwa watu wote.
- Wanachama wa kuomba. Raia wa Tanzania ambao watapenda kuwa wanachama wa Mandela Veteran Football Club wataomba kuwa wanachama na kupewa masharti ya kujiunga kulingana na vigezo vya katiba hii.
- Wanachama wa heshima. Wale wote waliopewa uanachama wa heshima kutokana na mchango wao katika Mandela Veteran Football Club hawatakuwa na haki ya kupiga kura
Sifa za kuwa mwanachama
Uanachama utatolewa kwa mwombaji ambaye:
- Awe na umri usiopungua miaka 18.
- Awe na akili timamu.
- Mwenye nia na lengo moja la kudumisha ustawi wa jumuiya yetu kwa kuwajibika ipasavyo.
- Aliyekuwa tayari kufata taratibu na sera za Mandera Veterans kulingana na katiba hii.
Utaratibu wa kupata hadhi ya uanachama
- Mwombaji atatakiwa kutuma maombi ya kujiunga uanachamawa Mandela Veteran Football Club na kuwasilisha kwa katibu Mkuu wa klabu.
- Maombi yataambatanishwa na:-
- Fomu iliyojazwa kikamilifu itakayotolewa na Klabu
- Kiingilio cha uanachama na ada ya kila mwezi iliyoidhinishwa na Bodi ya Utendaji
- Tamko linalosema kwamba anakubali kufuata Katiba hii, kanuni, masherti na maagizo/maelekezo ya Klabu katika muundo wake na pia maamuzi ya SUFA, FARU na TFF pamoja na ligi zinazounda vyama hivyo
- Tamko kwamba anatambua mamlaka ya Baraza la usuluhishi kuhusiana na migogoro yote ya kisheria inayohusu masuala ya mpira wa miguu
- Mwombaji akikubaliwa kujiunga na chama atalipa kiingilio Shilingi gharama mbalimbali ikiwepo kiingilio.
Bodi tendaji ya Mandela Veteran Football Club ndiyo yenye mamlaka ya kuyapokea maombi ya uanachama kuyajadili na kuyapeleka mapendekezo yake kwenye Mkutano Mkuu.