Ufafanuzi wa Muundo
- Mkutano Mkuu ni mkutano ambao wanachama wote wa Klabu watakutana na utawakilisha mamlaka ya juu ya Klabu. Huu ni mkutano ulioitishwa kwa kufuata utaratibu uliowekwa na utakuwa na mamlaka ya kufanya maamuzi
- Hali kadhalika, watakaoitwa katika Mkutano Mkuu huo kama washauri ni wanachama wa heshima watakaoteuliwa na Bodi ya utendaji
- Bodi ya utendaji itaamua kuhusu ushiriki wa wasio Hata hivyo hawatakuwa na haki ya kupiga kura ingawa wataombwa kutoa ushauri kwa idhini ya Mwenyekiti wa Mkutano
Wajumbe wa Mkutano Mkuu
- Mkutano Mkuu wa Klabu utakuwa na wajumbe wafuatao:
- Wajumbe wa Bodi ya utendaji
- Wanachama kamili wote
- Wanachama wa heshima
- Wajumbe wengine kama itakavyoamuliwa na Mkutano Mkuu
Kila mjumbe halali wa Mkutano Mkuu wa Klabu lazima awe na kadi halali ya uanachama iliyotolewa na Klabu. Sekretarieti ya Klabu itawaomba wajumbe kuonyesha nyaraka hizo kwa ajili ya uthibitisho.
Maeneo ya Mamlaka
Pamoja na mambo mengine Mkutano Mkuu utakuwa na maeneo ya mamlaka kama ifuatavyo:
- Kupitisha Katiba na kanuni zinazosimamia matumizi yake kama ilivyopendekezwa na Bodi ya utendaji
- Kuthibitisha kumbukumbu za mkutano uliopita
- Kupitisha bajeti ya mwaka au muda uliopangwa kwa mujibu wa Katiba hii ya shughuli na mipango ya Klabu
- Kuthibitisha hesabu za mwaka au muda uliopangwa kwa mujibu wa Katiba hii na kujadili kuhusu mafungu ya fedha za ziada au kutoa taarifa kuhusu namna nakisi inayotokana na taarifa ya mapato itakayofidiwa
- Kuthibitisha taarifa ya shughuli za Bodi ya utendaji
- Kuthibitisha rasmi hatua zilizochukuliwa na Bodi ya utendaji baada ya kusikiliza taarifa za hesabu kutoka kamuni ya ukaguzi wa hesabu
- Kuthibitisha hesabu zilizokaguliwa kwa kila mwaka
- Kuteua Bodi ya utendaji
- Kuamua kuhusu pendekezo la Bodi ya utendaji kupewa hadhi ya mmwanachama wa heshima kwa mtu aliyetoa mchango mkubwa sana kwa mpira wa miguu ndani ya Mandela Veteran Sports Club
- Kuidhinisha kujiuzuru kwa mwanachama
- Kumwandikisha mwanachama aliyejiuzuru
- Kutoa au kubadilisha mamlaka ya mwanachama mmoja au zaidi wa chombo cha Klabu
- Kuvunja Klabu ya mpira ya Mandela Veteran Sports Club