Ufafanuzi wa Muundo

  • Mkutano Mkuu  ni  mkutano  ambao  wanachama  wote  wa  Klabu  watakutana  na  utawakilisha mamlaka   ya  juu  ya Klabu.  Huu   ni  mkutano  ulioitishwa  kwa  kufuata  utaratibu  uliowekwa  na  utakuwa  na  mamlaka   ya  kufanya  maamuzi
  • Hali kadhalika,  watakaoitwa  katika  Mkutano  Mkuu  huo  kama  washauri  ni  wanachama  wa  heshima  watakaoteuliwa  na  Bodi  ya  utendaji
  • Bodi ya  utendaji  itaamua  kuhusu  ushiriki  wa  wasio    Hata  hivyo  hawatakuwa  na  haki  ya  kupiga  kura  ingawa  wataombwa  kutoa  ushauri  kwa  idhini   ya  Mwenyekiti  wa  Mkutano

Wajumbe wa Mkutano Mkuu

  • Mkutano Mkuu wa Klabu utakuwa na wajumbe wafuatao:
  • Wajumbe wa Bodi ya utendaji
  • Wanachama kamili wote
  • Wanachama wa heshima
  • Wajumbe wengine kama itakavyoamuliwa na Mkutano Mkuu

Kila  mjumbe  halali  wa  Mkutano  Mkuu wa  Klabu  lazima  awe  na  kadi  halali  ya  uanachama  iliyotolewa   na  Klabu.  Sekretarieti  ya  Klabu  itawaomba  wajumbe  kuonyesha nyaraka  hizo  kwa  ajili  ya  uthibitisho.

Maeneo ya Mamlaka

Pamoja  na  mambo  mengine  Mkutano  Mkuu  utakuwa  na  maeneo  ya  mamlaka kama  ifuatavyo:

  • Kupitisha Katiba  na  kanuni  zinazosimamia  matumizi  yake  kama  ilivyopendekezwa  na  Bodi  ya  utendaji
  • Kuthibitisha kumbukumbu  za  mkutano  uliopita
  • Kupitisha bajeti  ya  mwaka au  muda  uliopangwa  kwa  mujibu  wa  Katiba  hii ya shughuli  na  mipango  ya  Klabu
  • Kuthibitisha hesabu  za  mwaka  au  muda  uliopangwa  kwa  mujibu  wa  Katiba  hii  na  kujadili  kuhusu  mafungu  ya  fedha  za ziada  au  kutoa  taarifa  kuhusu  namna  nakisi  inayotokana  na  taarifa  ya  mapato  itakayofidiwa
  • Kuthibitisha taarifa ya  shughuli  za  Bodi  ya  utendaji
  • Kuthibitisha rasmi  hatua  zilizochukuliwa  na  Bodi  ya  utendaji  baada  ya  kusikiliza  taarifa  za  hesabu kutoka  kamuni ya  ukaguzi  wa  hesabu
  • Kuthibitisha hesabu  zilizokaguliwa  kwa  kila  mwaka
  • Kuteua Bodi ya  utendaji
  • Kuamua kuhusu  pendekezo la  Bodi  ya  utendaji  kupewa hadhi  ya  mmwanachama  wa  heshima  kwa  mtu  aliyetoa  mchango  mkubwa sana  kwa  mpira  wa  miguu  ndani  ya  Mandela  Veteran  Sports  Club
  • Kuidhinisha kujiuzuru  kwa  mwanachama
  • Kumwandikisha mwanachama  aliyejiuzuru
  • Kutoa au  kubadilisha  mamlaka  ya  mwanachama  mmoja  au  zaidi  wa  chombo  cha  Klabu
  • Kuvunja Klabu  ya  mpira  ya  Mandela  Veteran  Sports  Club
mandela
January 25, 2022

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *