Kila mwanachama wa Klabu atakuwa na wajibu ufuatao:

  • Kulipa kiasi chote cha fedha anachodaiwa na Klabu pamoja  na  michango
  • Kuwa mwaminifu na mtiifu kwa Klabu
  • Kukubali kufuata Katiba hii, kanuni, maagizo na maamuzi  ya  Klabu  na  ya  vyama  vya  mpira  wa  miguu  (SUFA, FARU  na TFF)
  • Kufuata kifungu cha sheria kinachoeleza bayana kuwa hatua zote za kisheria zinazohitaji kuamua migogoro inayohusu yeye au mwanachama mwingine  na  kuhusiana  na  Katiba, kanuni,  maagizo  na  maanuzi  ya  Klabu na  kwamba  ni  lazima  iwe  kwa  mujibu  wa  mamlaka  pekee  ya  Baraza la  usuluhishi  litakalotoa  uamuzi
  • Kufuata masharti yaliyobainishwa katika ibara ya 6 katika kipindi chote cha uanachama wake
  • Kufuata misingi ya uaminifu, uadilifu na mwendo mzuri wa kimichezo kama kuonyesha mchezo safi
  • Wajibu mwingine wowote unaotokana na Katiba hii, kanuni, maagizo na maamuzi ya Mandela Veteran Football Club

Aidha wanachama wataheshimu wajibu ufuatao:

  • Watakubaliana kuitumia Bodi ya Utendaji ya Klabu,  Kamati  ya  nidhamu  ya  Klabu,  Kamati  ya  nidhamu  ya  TFF  na  Baraza  la  usuluhishi  la  TFF
  • Kutopeleka masuala ya mpira wa miguu katika mahakama ya kawaida ya sheria
  • Mwanachama au mtu yeyote (mchezaji au kiongozi) atakayetafuta  msaada  katika  mahakama  za  kawaida  ya  sheria  kuhusu  mgogoro  unaohusiana  na  Katiba,  kanuni,  taratibu,  maagizo  na  maamuzi  ya  Mandela  Veteran  Football  Club  atasababiishwa  kusimamishwa mara  moja  na  Bodi  ya  utendaji

Ibara ya 12: Kupoteza hadhi ya mwanachama

  • Hadhi ya mwanachama itakoma kwa kujiuzuru uanachama au kufukuzwa kutokana na ukiukwaji wa kanuni na sheria za katiba hii,TFF na sheria za nchi kwa ujumla.
  • Kupoteza uanachama hakutamwondolea mwanachama huyo   madeni yake katika Klabu au kwa wanachama wemgine wa chombo hicho
  • Kufariki, Mwanachama wa kudumu anapofariki, uanachama wake utakoma, lakini haki zake kikatiba atapewa mrithi wake halali ambaye atakuwa na hiyari ya kuendeleza uanachama kwa kwa mujibu wa masharti haya.
  • Kichaa kilichothibitishwa na daktari kama ilivyoelezwa kwenye kipengere cha Ibara ya 6(b).
  • Kujiuzulu baada ya kutoa taarifa ya maandishi miezi mitatu kabla, mwanachama wa kudumu anaweza kujitoa mwenyewe kwenye chama kwa sababu atakazoona zinafaa.
  • Kwa kujitoa mwenyewe atakuwa amejifuta kwenye uanachama wa kudumu au mkataba na kurudishiwa stahiki zake zote na kila kila kitu alichokuwa anapata kitakoma siku hiyo hiyo.
  • Kukataliwa uanachama na theluthi mbili (⅔) ya wanachama waliohudhuria katika Mkutano Mkuu baada ya kupewa nafasi ya kujitetea baada ya kufanya makosa ambayo yanamlazimu kukataliwa uanachama. Mfano Kupigana au tabia zingine zisizokuwa za utu.
  • Kufanya kitendo chochote ambacho wanachana na uongozi kwa ujumla wataridhika kuwa ni cha kutokuwa mwaminifu au ambacho ni kinyume na madhumuni ya jumuiya na ambacho kinavuruga malengo ya chama.
  • Kutoshiriki katika shughuli za chama kwa muda wa miezi mitatu (3) bila taarifa ya yeyote.
  • Mwanachama ambaye uanachama wake umekoma hatarudishiwa kiingilio alichotoa. Iwapo hadaiwi na chama atarudishiwa hisa zake zote baada ya miezi mitatu kupita tangu siku uanachama ulipokoma.
  • Kukosa sifa baada ya kushindwa kutimiza masharti ya kulipa michango ya kila mwezi kwa muda wa miezi mitatu (3) mfurulizo.
mandela
November 25, 2020

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *