Aina za wanachama Kutakuwa na aina zifuatazo za wanachama: Wanachama waanzilishi. Uanachama utakuwa wa wazi kwa watu wote. Wanachama wa kuomba. Raia wa Tanzania ambao watapenda kuwa wanachama wa Mandela Veteran Football Club wataomba kuwa wanachama na kupewa masharti ya kujiunga kulingana na vigezo vya katiba hii. Wanachama wa heshima. Wale wote waliopewa uanachama wa …
Mandela Veteran Football Club itakuwa na vyombo vifuatavyo: Mkutano Mkuu Bodi ya utendaji Sekretarieti Kamati za kudumu Kamati ya nidhamu Kamati ya uongozi Chombo cha ukaguzi wa mahesabu Bodi ya utendaji ina mamlaka ya kuteua kamati za kudumu, na kamati hizo ni za ushauri zitakazoongozwa na kanuni maalumu zitakazothibitishwa na Bodi ya utendaji Endapo dharura …
Ufafanuzi wa Muundo Mkutano Mkuu ni mkutano ambao wanachama wote wa Klabu watakutana na utawakilisha mamlaka ya juu ya Klabu. Huu ni mkutano ulioitishwa kwa kufuata utaratibu uliowekwa na utakuwa na mamlaka ya kufanya maamuzi Hali kadhalika, watakaoitwa katika Mkutano Mkuu huo kama washauri ni wanachama wa heshima watakaoteuliwa na Bodi ya utendaji Bodi ya …
Kila mwanachama wa Klabu atakuwa na wajibu ufuatao: Kulipa kiasi chote cha fedha anachodaiwa na Klabu pamoja na michango Kuwa mwaminifu na mtiifu kwa Klabu Kukubali kufuata Katiba hii, kanuni, maagizo na maamuzi ya Klabu na ya vyama vya mpira wa miguu (SUFA, FARU na TFF) Kufuata kifungu cha sheria kinachoeleza bayana kuwa hatua zote za kisheria zinazohitaji…
Kamati ya ufundi na tiba Kamati ya ufundi na tiba itachambua vipengere vya msingi vya maendeleo ya ufundi ya mchezo wa mpira wa miguu. Itaandaa mpango wa maendeleo, kufuatilia utekelezaji na kufanya tathimini ya mara kwa mara ya mafanikio au vikwazo katika mchezo wa mpira wa miguu na Klabu kwa ujumla. Pia itashughulika na masuala …
Mwanachama anaweza kujifuta uanachama kwa kuwasilisha barua kwa Katibu wa Klabu. Kufukuzwa uanachama Mkutano Mkuu unaweza kumfukuza mwanachama kutokana na ukiukwaji waKatiba hii, kanuni, maagizo na maamuzi ya Mandela Veteran Football Club kulingana na vigezo vilivyoainishwa kwenye Ibara ya 13 hapo juu.