Aina za wanachama

Kutakuwa na aina zifuatazo za wanachama:

  • Wanachama waanzilishi. Uanachama utakuwa wa wazi kwa watu wote.
  • Wanachama wa kuomba. Raia wa  Tanzania  ambao  watapenda  kuwa  wanachama  wa  Mandela  Veteran  Football  Club wataomba  kuwa  wanachama  na  kupewa  masharti ya  kujiunga  kulingana na vigezo vya katiba hii.
  • Wanachama wa heshima. Wale wote  waliopewa  uanachama  wa  heshima  kutokana  na  mchango  wao  katika  Mandela  Veteran  Football  Club  hawatakuwa  na  haki  ya  kupiga  kura

Sifa za kuwa mwanachama

Uanachama utatolewa kwa mwombaji ambaye:

  • Awe na umri usiopungua miaka 18.
  • Awe na akili timamu.
  • Mwenye nia na lengo moja la kudumisha ustawi wa jumuiya yetu kwa kuwajibika ipasavyo.
  • Aliyekuwa tayari kufata taratibu na sera za Mandera Veterans kulingana na katiba hii.

Utaratibu wa kupata hadhi ya uanachama

  1. Mwombaji atatakiwa kutuma maombi ya kujiunga uanachamawa Mandela Veteran Football Club na kuwasilisha kwa katibu Mkuu wa klabu.
  2. Maombi  yataambatanishwa  na:-
  1. Fomu iliyojazwa  kikamilifu  itakayotolewa  na  Klabu
  2. Kiingilio cha  uanachama  na  ada  ya  kila  mwezi  iliyoidhinishwa  na  Bodi  ya  Utendaji
  3. Tamko linalosema  kwamba  anakubali  kufuata  Katiba  hii,  kanuni,  masherti  na  maagizo/maelekezo  ya  Klabu  katika muundo  wake na  pia  maamuzi  ya  SUFA,  FARU  na  TFF  pamoja  na   ligi  zinazounda  vyama  hivyo
  4. Tamko kwamba  anatambua  mamlaka  ya  Baraza  la  usuluhishi  kuhusiana  na  migogoro  yote  ya kisheria inayohusu  masuala  ya  mpira  wa  miguu
  5. Mwombaji akikubaliwa kujiunga na chama atalipa kiingilio Shilingi gharama mbalimbali ikiwepo kiingilio.

Uamuzi   wa uanachama

Bodi tendaji  ya Mandela  Veteran  Football  Club  ndiyo  yenye  mamlaka  ya  kuyapokea  maombi  ya  uanachama  kuyajadili  na  kuyapeleka  mapendekezo  yake  kwenye  Mkutano  Mkuu.